YOU ARE NOT ALONE

"I can’t give solutions to all of life’s problems, doubts, or fears. But I can listen to you, and together we will search for answers."

karibuni

Karibuni katika blog yetu ambayo itakuwa ikizungumzia kuhusu masuala ya uzazi hasa kwa wale wenye matatizo ya kuchelewa kupata watoto (infertility). Hapa tutajadili chanzo cha matatizo hayo na njia zinazoweza kutumika kuondoa tatizo hilo pamoja na kupeana ushauri na nasaha katika masuala mbalimbali yanayohusu uzazi. "KWA NEEMA YA MUNGU KILA MWANAMKE ATANYONYESHA"

Friday 8 June 2012

MYTH & MISCONCEPTIONS

Myth: We should be having intercourse every day to achieve pregnancy.

Fact: Sperm remain alive and active in woman's cervical mucus for 48-72 hours following sexual intercourse; therefore, it isn't necessary to plan your lovemaking on a rigid schedule. Although having sexual intercourse near the time of ovulation is important, no single day is critical. So, don't be concerned if intercourse is not possible or practical on the day of ovulation.
Thanks to Dr. Malpani

MWEZI WA WASAKA DUNIANI

Katika post za mwanzoni niliwahi kueleza kuwa kuna  mwezi wa wasaka duniani, ambapo lengo kuu ni kutumia mwezi huu kusambaza elimu kwa jamii, kupeana faraja na kusaidiana kwa kila hali katika kupambana na tatizo la kukosa uzazi. baadhi ya nchi hutoa huduma za matibabu bure kwa wahitaji ama kupunguza kiwango cha malipo katika kutoa mchango wao kwa mwezi huu.
Katika kuzingatia umuhimu wa mwezi wetu huu nami nimeona  ni vizuri kuupa nafasi ya kipekee na kwa kuelimishana mambo mbali mbali yanayohusu kukosa uzazi (infertility). Hivyo basi napenda kutambulisha vipengele vipya ambavyo vitakuwa vinaelezea mambo mbali mbali yatakayotupa uelewa mzuri. Vipengele vipya ni kama ifuatavyo:- 

-FAHAMU KUKOSA UZAZI (INFERTILITY) - Tumekuwa tukiongea sana kuhusu suala hili la kukosa uzazi,  kusaka mtoto, kutafuta matibabu na mengineyo lakini je tunaelewa kwa undani maana yake, chanzo chake, na matibabu yake? kipengele hiki kitaelezea kwa undani kuhusu suala hilo.

-JINSI YA KUKABILIANA NA KUKOSA UZAZI (JKKU) - Hapa tutaeleza njia mbali mbali zinazoweza kumsaidia msaka kukabiliana na kupambana na hali halisi ili kuweza kumpunguzia machungu anayokutana nayo kwenye safari hii.

-NI CHAGUO LAKO, NI WAKO - Katika post zetu tunaongelea sana kuhusu kutafuta matibabu ili kuweza kupata mtoto wa kuzaa mwenyewe, lakini kuna wasaka wenzetu ambao wapo katika hali ambayo kupata mtoto wa kuzaa mwenyewe ni hali ngumu kidogo, ili kuwapa nafasi na kuwa pamoja nao kipengele hichi kitasaidia katika kufanya maamuzi pale mtu anapohitaji kuasili (adoption) mtoto. Na hivyo tunasema ni chaguo lako, ni wako.

-INFERTILITY NEWS - Hapa tutapata habari mbali mbali zinazohusu infertility zinazotokea sehemu yoyote duniani, lengo ni kupeana taarifa na kwenda na wakati kwa maendeleo yoyote yanayotokea duniani

-MYTH & MISCONCEPTION - Kumekuwa na mawazo tofauti yanayoelezwa kuhusu chanzo cha kukosa uzazi na matibabu yake ambayo yanajenga imani potofu katika jamii. kipengele hichi kitaelezea na kutoa ukweli wa mawazo hayo.

-ZIFAHAMU DAWA UTUMIAZO - Katika safari ya usaka tunatumia dawa za aina mbali mbali, lakini ukweli ni kwamba asilimia kubwa ya watanzania hatuna maelezo ya kutosha ya dawa tunazotumia na jinsi gani dawa hizo zinatusaidia, katika kipengele hiki utayapata yote hapo. Infertility Fighter kwa ajili yako.

ULIWAHI KUFAHAMU KAMA KUNA RIBBON INAYOHUSU INFERTILITY?? KAMA BADO  ICHEKI HAPO CHINI. KITU BLUE NA PINK (nadhani wanawakilisha boy na girl tunaowasaka). Nimeipenda na nitaitafutia nafasi kwa hapo juu niiweke