YOU ARE NOT ALONE

"I can’t give solutions to all of life’s problems, doubts, or fears. But I can listen to you, and together we will search for answers."

karibuni

Karibuni katika blog yetu ambayo itakuwa ikizungumzia kuhusu masuala ya uzazi hasa kwa wale wenye matatizo ya kuchelewa kupata watoto (infertility). Hapa tutajadili chanzo cha matatizo hayo na njia zinazoweza kutumika kuondoa tatizo hilo pamoja na kupeana ushauri na nasaha katika masuala mbalimbali yanayohusu uzazi. "KWA NEEMA YA MUNGU KILA MWANAMKE ATANYONYESHA"

Tuesday 28 February 2012

Kauli Mbiu

Wadau,
kuna mdau anony wa pili kuchangia kwenye STORY YANGU -1 alitoa maoni yake mwisho akasema atasapoti ili "kila mwanamke anyonyeshe"   mnaonaje hayo maneno niliyopigia mstari tuyaongezee maneno  kidogo na ikawa ndio kauli mbiu yetu? nipeni mawazo yenu

Story Yangu -3

nilitumia metformin kwa miezi sita bila mafanikio na nikaanza kukata tamaa, hasa baada ya mume wangu kupata nafasi ya masomo nje ya nchi. hapo sasa niliona mimi kuzaa ndio historia nitaishia kuitaja tu na hata zile dawa nikaacha kutumia.

kwa bahati nzuri safari yake haikuwa kikwazo sana kwani alikuwa akirudi nyumbani mara kwa mara, aliondoka mwishoni september na december akarudi hivyo haikuniathiri sana. Hapo sasa nilirudi hospitali na nikapewa dawa za aina 2, kuna ambazo unakunywa kila siku na zingine ndio zile unakunywa MP tu ikiisha kuhesabu siku. nilikuwa nakunywa kila akiwa anarudi tanzania, nazo pia sikufanikiwa, nikaambiwa sasa inabidi nifanyiwe opareshen kuangalia kama kuna ukungu utolewe!!!! nini!!! opareshen kuangalia kama kuna ukungu!!!? kama huo ukungu upo sawa itakuwa nimepata tiba, kama haupo je???!!!! mmh ilikuwa ngumu kuamua kwa kweli kupasuliwa kwa majaribio... hapana moyo uligoma, sikurudi kupasuliwa. baada ya hali hiyo mwezi december 2007 nikaamua kusafiri nami nikiwa na tamaa walau nitapata matibabu zaidi.

nilienda hospitali ya kwanza, nilieleza historia yangu yote na kufanyiwa vipimo. daktari akasema kuwa haoni tatizo lolote kila kitu kipo sawa. hakunipa hata  dawa ya maumivu, ila alinielekeza niende hospitali nyengine kwa daktari bingwa zaidi. nakumbuka huyu mama aliniambia maneno ambayo yalinitia nguvu sana, naomba ninukuu baadhi ya maneno aliyoniambia kwa faida ya wanawake wenzangu.

alisema hivi " najua unaumia kwa sasa, lakini jaribu kuishi hizi siku zako kwa raha zote kwani utakapoanza kupata watoto utaukumbuka huu muda na kutamani urudi tena" (ni kweli unaitamani ile free time baada ya majukumu kuongezeka, ingawa faraja ya kuwa mama inakupa nguvu ya kupambana na maisha) alisema yeye alipata mtoto wa kwanza akiwa na miaka 38 

basi, nikaenda hospitali nyengine ambako ni kwa gyno bingwa, naye pia alinipima na kuniambiwa kuwa haoni tatizo lolote kila kitu kipo sawa sawa. akanipima na matiti akasema matiti yangu yanaonesha ninao uwezo wa kuzaa. nako sikupewa dawa, sasa nikawa najiuliza ile PCOS imeenda wapi? au ndio zile dawa zilinisaidia? lakini mbona wanasema PCOS huwa haiponi? sijui na mpaka sasa bado sijapata hili jawabu. nikarudi zangu Tz nikiwa na maswali mengi kichwani ingawa nilikuwa na tamaa baada ya yale majibu ya madaktari. 

hapo sasa niliamua kujitibia mwenyewe, nilishachoka na safari za hospitali kila siku. nilikuwa kama kichaa nusu mwendawazimu, nalala na mtandao naamka na mtandao, nilitafuta kila kitu kinachohusiana na uzazi,  matatizo, chanzo chake ma matibabu, ingelikuwa kutibia watu sio lazima ukasome vyuoni basi mimi ningebadilisha utaalamu na kuwa gyno. ilifika wakati hata nikiwa njiani niko na makaratasi yangu nasoma.

niliendelea kutafuta suluhisho  hadi mwishoni mwa 2008 ndio nikakutana na hiyo siri yetu. nashukuru mungu mwezi huo huo mambo yakawa mazuri na August 2009 nikajifungua mtoto wa kiume.

mwaka 2010 nilipata ujauzito mwingine na ilikuja tu yenyewe bila kutegemea lakini niilipata bahati mbaya ikiwa na miezi miwili. nikaamua kupumzika. sasa natamani mtoto wa pili ambapo nimejaribu kawaida mpaka sasa bila mafanikio, na nataka kuirudia siri yetu..............

nimejifikiria mimi na pia kuwafikiria wenzangu ambao nao ni wahanga, ndio nikaona bora kuanzisha blog ili tupate sehemu yetu ya kupeana mawazo, ushauri na kupeana moyo. kwa wale wote wasaka wenzangu twende pamoja.....................tutaiona njia kwa uwezo wa mungu.

na kwa nyote mliobarikiwa tunawahitaji kwa msaada wa mawazo na ushirikiano ili tupate nguvu ya kupambana na majaribu haya.

kwa anaetaka kujua hiyo siri tuwasiliane kwa email yangu sanraznassy@hotmail.com muda wowote. 

Monday 27 February 2012

Story Yangu -2

safari yangu ilianzia miezi michache baada ya kufunga ndoa, kusema kweli ile miezi sita ya mwanzo sikuwa na wasiwasi sana hasa kwa vile niliolewa mara tu baada ya kumaliza mitihani ya mwisho ya chuo, hata kabla ya graduation hivyo kulikuwa na kipindi cha kufanya mazoezi kwa vitendo (field) na muda wa kutafuta kazi, kwangu niliona sawa tu nikipata au nisipopata kwa wakati ule kwavile nilikuwa bado najipanga kimaisha.

baada ya miezi sita kupita ukizingatia kuwa sikuwahi kutumia njia yoyote ya uzazi katika maisha maisha yangu ndio sasa nikaanza kuwa na wasi wasi ingawa pia bado wakati huo sikuwa na ile presha saaana  ya kupata mtoto, basi katika kuongea na familia yangu kuhusu jambo hilo wakanipatia dawa za kiasili nikumie tukiamini kuwa zitasaidia, nilitumia kama miezi minne mfululizo bila mafanikio yoyote.

hapo sasa ndio hofu ikaningia, huyo mbio mpaka hospitali (naomba nihifadhi jina la hospitali hii ili kulinda heshima yao, inawezekana sikufanikiwa mimi ila wapo waliofanikiwa hapo hapo kwani matatizo hayalingani) nilikutana na daktari akaniandikia dawa na kurudi zangu nyumbani, baada kutumia dawa hizo tatizo jipya kijitokeza, nikaaza kubleed haikuwa nyingi sana ila ilikuwa ya muda mrefu nilibleed kwa zaidi ya miezi tisa mfululizo, ilikuwa ikiacha labda siku moja yapili inarudi tena, au napumzika asubuhi jioni tena, basi hayo yakawa ndio maisha yangu kwa takriban mwaka mzima. nilikosa raha jamani nikasema mimba sipati sasa hiki nini tena jamani. Ukiniuliza ni dawa gani ilinisaidia siijui maana nilikunywa kila kilicholetwa mbele yamgu, vidonge vya hospitali, majani hadi mizizi nahangaika kutafuta uzima wangu. nashukuru mungu nilipona mwanzoni mwa mwaka 2006.

katika hangaika yetu mwaka huohuo 2006 tulipata habari za kuanzishwa kwa kituo ama clinic ya kina mama katika hospitali ya Muhimbili. ilikuwa ikiitwa WELL WOMAN CLINIC, ilikuwa ni kitengo maalum cha kuwapima na kuwatibia kina mama tu, na huduma zao zilikuwa ni nzuri sana sijui ni kwanini waliacha kikafa kile kitengo. Basi nikafika hapo na kuhudumiwa vizuri sana. walinifanyia vipimo vyote hadi kansa ya kizazi, baada ya kuridhika na majibu ya awali nikapangiwa gyno ambaye alinitaka nifanye vipimo vya ziada viwili, nilipima  mirija na kukuta iko sawa, nikafanya ultra-sound ambayo ilionyesha kuwa nina PCOS. basi matibabu yakaanza, aliniandikia METFOMIN ( vidonge hivi hutumia na wagonjwa wa kisukari ndio dawa yao kubwa) ambayo nilitakiwa kunywa kwa miezi mitatu kama ikipita hiyo sijafanikiwa basi nirudi tena hospitali.

ANGALIZO: ingawa metfomin ni dawa za wagonjwa wa kisukari ila zinatumika sana kutibu PCOS ni moja kati ya dawa kuu zinazotegemewa kwani PCOs inahusiana na insulin resistance. 
kwa wale wenye PCOS mnaweza kutembelea mtandao huu ambao ni kama forum kwa watu wenye PCOS  tu, hapo unaweza uliza swali lolote ukapata majibu,  inaweza kuwasaidia  www.soulcysters.com

 xxxxxxxxxxxxxxx narudi sasa hivi...................................


Saturday 25 February 2012

just a moment please

Wapendwa,
naomba mnivumilie kidogo tu muda si mrefu nitamalizia story yangu. nimepokea malalamiko mengi kuhusu kutomalizia story, naomba tuelewe kuwa lengo hapa ni kumsaidia mwanamke kwa kila njia, naweza kuandika story kwa mistari mitatu tu na nikamaliza, sawa itasaidia lakini sio wote kwani nitasema tu ilikuwaje nilifanya nini na ikawa nini. wakati kuna mwanamke mwenzetu ambaye yupo kwenye hali ngumu kumtoa hapo alipo na kumwambia aamini matokeo yako ni ngumu, pia lengo ni kusaidiana kupata kizazi na pia kimawazo na nasaha hata kwa wale ambao hawawezi kupata tena watoto.

pia tukumbuke kuwa blog yetu inagusa hisia nzito za watu, watu walioumia na wengine hata kukata tamaa ya maisha hivyo inabidi kujipanga kwa kila tutakaloongea ili mdau alipokee vizuri na liwe la msaada kwake ni kama mfano wa mtu mwenye ulemavu wa macho ukakurupuka na kumuita kipofu ni lazima ataumia ila ukitumia hilo la kwanza atakuelewa, hivyo uchaguzi wa maneno au lugha safi pia unachangia kuchelewa huko.

jambo lingine ni kuwa hapa naongelea historia ya maisha ya ukweli na sio hadithi ya kutunga wala maigizo ambayo inashirikisha watu wengi, inabidi kuwa makini pia na maelezo kwani pamoja na kuwa wapo na wanatukwaza kwa shida zetu hizi lakini bado pia watu hao ni sehemu ya maisha yetu na jamii inayotuzunguka hivyo pamoja na yote tunahitaji kuwa na mahusiano mema nao.

naomba tushirikiane kwa wale wote wenye maoni, michango au ushuhuda mniandikie kupitia e-mail yangu sanraznassy@hotmail.com nami nitayaweka hadharani ili kila mwanamke afaidike. muda si mrefu nitatoa namba ya simu tuwasiliane.

kwa wale wanaohitaji kujua siri yangu pliz nitumieni email pia mniandikie na contact zenu tutawasiliana. sio siri kubwa ila napenda kuongea nanyi private ili kulinda heshima za watu mbali mbali akiwemo mwenza wangu.

tushirikiane, pamoja tutashinda.

Msapoti mwenza wako


tatizo la kushindwa kupata ujauzito linaweza kutokana na mwanamke au mwanaume, inaweza kuwa wote kwa pamoja au sababu nyenginezo. mara nyingi tatizo likiwa kwa mwanaume, mwanamke huwa na uvumilivu na upendo, humsubiria mwenziwe mpaka kieleweke!!! (ingawa wapo wachache wasioweza kuvumilia), lakini hali huwa tofauti iwapo tatizo ni la mwanamke. Ukweli ni kwamba ni wanaume wachache sana wanaoweza kuwavumilia na kuwasapoti wenza wao. wengi wao hushindwa kutokana na presha za familia zao au mazingira yanayowazunguka. wanachosahau ni kuwa kile kitendo cha kumnyanyapaa mwenzi wako kinaweza kuwa ndio sababu kubwa ya nyinyi kukosa mtoto kwani mwanamke huishia kuwa na msongo wa mawazo muda wote....



 kila mtu kivyake......



hupunguza upendo kwa kweli na humfanya mwanamke ajione kama ni mkosaji wakati hana hatia yoyote.
Daima kumbuka upendo wako ndio utakaomtia nguvu za kupambana na majaribu hayo.



cheki inavonoga mkiongozana wote kutafuta suluhisho

na kuyapokea majibu kwa pamoja jee!!!


jamani ni upendo wa hali ya juu. hata kama ni negative pliz kuwa karibu nae kwani anakuhitaji zaidi ya unavyofikiria. kuwa baba ni fahari kwako na jamii lakini kuwa mama pia ni life time experience ambayo kila mwanamke anaihitaji. sio kosa lake laiti ungejua ni kiasi gani anaumia kwa majibu hayo hayo yanayokukera wewe ungeisimamisha hata dunia isitembee mpaka machungu ya mwenzako yapungue.


usipomsaidia sasa hivi utajisikiaje siku mambo yakiwa mazuri?

siwezi kuimagine utakavyokuwa unajieleza..... oh darling nilijuwa tu tutafanikiwa. au mpenzi nimekuwekea pesa za shopping kwa ajili yako na baby wetu. duh hebu simama sasa na uchukue nafasi yako, mpende na umsapoti ili mambo yakijipa uwe proud kikweliiii hata ukijamuhadithia mwanao jinsi mlivyosubiri huwi na majuto


pliz show love...



daima kumbuka, anaumia kama wewe na anakuhitaji zaidi wewe ndio nguzo ya ujasiri na nguvu zake kwa pamoja mtayashinda majaribu, pliz do it for her na huyo baby unaemtamani....

napenda kuchukua nafasi hii kuwapa hongera wale wote wanaowafariji na kuwatia moyo wenza wao. huo ni ujasiri na kutimiza ahadi yako ya kumlinda, kumheshimu na kumpenda. naamini dini au imani zote wanazingatia hili wakati wanapofungisha ndoa, kwa waislamu huhimizwa kuwa na mapenzi (mawadda) kwa wake zao pamoja na huruma na wakristo pia huhimizwa mapenzi tena na viapo kupeana for better for worse. na imani zote nyinginezo naamini wanazingatia hili.


Monday 20 February 2012

JIACHIE : Negative Test Result

Hivi mdau unajisikiaje pale unapokuwa na tamaa na ikifika mwisho wa mwezi unakuta kitu holaaaaa!!!!
JIACHIE... hii ni sehemu ya kutoa dukuduku lako moyoni, ili wadau wakusikilize na kukupa ushauri, mawazo na kukutia moyo. Usijali mpendwa hauko peke yako na kumbuka iko siku zamu yako itafika

Thursday 2 February 2012

Story Yangu - 1


Kawaida binaadamu tumeumbwa na tamaa, iwe ni ya afya, mali, watoto, vyeo na mengineyo na kila mtu kwenye ulimwengu ana kitu ambacho anakitamani. lakini wengi kati yetu hasa wanawake huwa na tamaa ya kupata mwenza  wako, mkaishi kama mke na mume na mpate watoto...... na tamaa hii iko wazi na wala haijifichi miongoni mwa wengi.

kati ya hao wanaotamani mimi ni mmoja wapo, tamaa yangu ilianza mwaka 2004 baada ya kufunga ndoa, nilianza kuhesabu.... siku zikapita........miezi ikakata! na miaka ikapotea.!!!! lakini sikubarikiwa. what is wrong????  nilianza kujiuliza. Kufikia hapo tamaa  iligeuka ikawa ni mawazo,  hasira na kila unachokijua ambacho mtu humtokea pindi unapokosa kitu fulani unachokihitaji  zaidi, hasa ikiwa jamii inayokuzunguka haikuelewi na inategemea utende mambo ambayo yapo nje ya uwezo wako na miujiza ambayo hujabarikiwa. Naamini kwa ambaye amewahi pitia njia hii au bado yupo kwenye njia hii ananielewa zaidi.

Kama mjuavyo, msaka hachoki na akichoka basi keshapata! basi nami huyooooo kiguu na njia ........ mara kusi mara kaskazi nikisaka nisichojaaliwa.

lol hebu acha nipumue kwanza maana hii safari ni ndefu .....................tutakutana tena